![]() |
|
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Teknolojia mpya ya Google map29/01/2009
Kampuni kubwa ya mtandao duniani (GOOGLE) imezindua teknolojia mpya ya kuchambua mitaa ya UK kwa wanaotumia Google map kupata picha halisi ya sehemu za UK uso kwa macho ukiwa katika kiti cha kompyuta yuko. Teknolojia hiyo ambayo inaitwa "Street View" inakupa sura ya mitaa ya UK pembe zote (360 degree) kama ukiwepo sehemu hiyo hai. Mtu yoyote ambaye yupo popote duniani akiandika anuani au 'post code' ya mahali pa London anaweza kupata picha halisi ya anuani hiyo na kumuezesha kuona nyumba, magari, watu na kila kitu kama vile yupo pale yeye mwenyewe hai na inakuezesha kuangalia sehemu hiyo pande zote (36 degree). Kwa sehemu ambazo hazijatiwa kwenye Google Map, Street View, zinatarajiwa kutiwa siku za mbele. Watu wataweza kutembelea Big Ben, Tower Bridge, London Eye bila ya kutoka nyumbani kwa kutumia teknolojia hiyo. Kuangalia inavyofanya kazi, bonyeza hapa na jaribu kuandika anuani upate picha halisi ya sehemu.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||