Wasanii wa UK kuupanda
mlima Kilimanjaro
03/02/2009

Wasanii wa fani mbalimbali wa UK
wamejitolea mchango wa kusaidia matatizo mbalimbali yanayowakuta watoto
na baadhi ya jamii barani Afrika.
Wasanii hao ambao wamepewa fursa na
kampuni ya BT (British Telecom) kwa kujitolea kwa njia ya mradi wa COMIC
RELIEF kuupanda mlima wa Kilimanjaro, Tanzania kuonyesha nia yao ya
kusaidia kukuza mfuko wa msaada uliokusudiwa.
Baadhi ya misaada kusudiwa ikiwamo
kupigana vita na magonjwa ya Malaria ambayo inaua wengi barani Afrika
kutokana na kuto kuwa na kinga (kama vyandarua na madawa).
Watakaoshiriki kuupanda mlima Kilimanjaro
ni kama wafuatao:

Alesha: Muimbaji, mwandishi wa
nyimbo, mtangazaji wa TV, mchezaji dansa.

Ben: Mtangazaji wa TV wa Channel 4
UK, na kapata umaarufu wake mkubwa hivi karibuni kwenye kipindi cha
X-Factor.

Cheryl: Muimbaji wa kikundi cha
Girls Aloud, na kapata umaarufu wake mkubwa hivi karibuni kwenye kipindi
cha X-Factor. Cheryl kaolewa na mchezaji maarufu wa England, Ashley Cole
ambaye pia ni beki tatu wa timu ya Chelsea.

Chris: DJ wa radio na vilevile ni
mtangazaji wa TV.

Denise: Mtangazaji wa TV na
muigizaji wa michezo mbalimbali kwenye salasila za TV, UK.

Fearne: Mtangazaji wa TV, na kapata
umaarufu wake mkubwa hivi karibuni kwenye kipindi cha X-Factor.

Gary: Muimbaji.

Kimberley: Muimbaji wa kikundi cha
Girls Aloud cha UK.

Ronan: Muimbaji wa kikundi cha
Boyzone cha UK.
|