Mahafali sekondari ya
Jamhuri, Dodoma
05/02/2009

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jamhuri kidato cha
sita wa shule ya Jamhuri, Dodoma, wakimsikiliza kwa makini Mhe. Abdallah
Omari Kigoda (hayupo kwenye picha) wakati alipokuwa akizungumza nao
baada ya kuwakabidhi vyeti vya kumaliza shule mjini Dodoma.

Mhe. Abdallah Omari Kigoda (watatu kulia) akimkabidhi
Cheti mwanafunzi wa kidato cha sita Ndugu Suleiman Ally cha kumaliza
kidato cha Sita, wa shule ya sekondari ya Jamhuri mjini Dodoma katika
sherehe ya mahafali ya kumaliza kidato cha sita ya shule hiyo. Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Ndugu Juma Kagoda akionekana pichani kulia.
|