Kizimbani kwa mauaji
13/02/2009

Watuhumiwa wa mauaji ya kutisha
yaliyotekea jijini hivi karibuni Vinoth Praveen (23) na mkewe Komal
Bupendra (23) wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam. Wanatuhumiwa kumuua Abdul Basit Abdallah kumkatakata na mwili
kuuweka katika begi na kuutelekeza ndani ya gari katika jengo la J. M.
Mall. Watuhumiwa hao walikuwa wakidaiwa kiasi cha dola za USA 20,000.

Vinoth Praveen, raia wa India, (23) aliyechuchumaa chini
kulia, kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara mwenzake, Abdulbasit
Abdallah (21), aliyechuchumaa kushoto, ambaye mwili wake ulikutwa ndani
ya begi la nguo katika Jengo la Harbour View Tower katika Mtaa wa Samora.
Aidha, inawashikilia kwa tuhuma hizo, mke wa Praven,
Komal Katakia (22), wakwe zake Bupindra Jerah (61) na Malti Bupindra
(46), pamoja na rafiki yake, Abraham Akbar (23) ambao ni raia wa
Tanzania wenye asili ya Kiasia.
|