Nyaya za Fibre Optics
zatandikwa
19/02/2009

Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa
wamebeba waya (fibre optic cable) ambao utawekwa katika kituo chao
kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma ya
mawasiliano ya kileo nchini. Toka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo
Michael Njumba akifuatiwa na Meneja Mkurugenzi Anna Rupia na kushoto ni
Muhandisi Jon Avery.

Wahandisi wa kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa
wanafunga kamba ili kuvuta waya ya mawasiliano (fibre optic cable)
kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa
katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited
wakionekana wakiwa wamebeba waya ya mawasiliano (fibre optic cable)
kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa
katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Mafundi ujenzi wakijenga kituo cha waya ya mawasiliano (
Fibre Optic Cable) cha Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited kilichopo
Kunduchi Jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo itaanza kutoa huduma hiyo ya
kuboresha network nchini mwezi wa sita mwaka huu.
|