Wakala wa ndege wailaza
timu ya mashirika ya ndege
24/02/2009

Mgeni rasmi Naibu waziri wa mawasiliano, utamaduni na
michezo wa Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akishiriki katika mchezo
wa kuvuta kamba katika tamasha la michezo lililoandaliwa na Galileo
Tanzania katika viwanja vya Leaders Club.

Katika mashindano hayo kulikuwepo na mashindano ya
michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbia kwa kutumia magunia, michezo ya
kamba na mingineyo.

Timu ya mawakala wa ndege iliwakandamiza kwa mashirika ya
ndege yaliyo Tanzania magoli 3-0 katika michezo iliyoandaliwa na Galileo
Tanzania, katika viwanja vya Leaders Club.
|