Uchaguzi Mkuu wa CUF 2009
25/02/2009

Profesa Lipumba akipongezwa na Mh. Hamad, kiongozi wa
upinzani bungeni, baada ya kuibuka mshindi wa uenyekiti wa chama cha CUF
katika uchaguzi mkuu wa 2009 uliohitimisha mkutano mkuu wa 4 wa chama
hicho katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es Salaam.

profesa lipumba alipata kura 600 kati ya kura 669
zilizopigwa na kuwashinda wagombea wengine wawili kwa asilimia 98.6.
Wagombea wengine Koplo Stephen Masanja alipata kura 10 (asilimia 1.5) na
Profesa Abdallah Safari aliyepata kura 6 (asilimia 0.9).

Maalim seif naye alizoa kura 657 (asilimia 99.5) za kiti
cha Ukatibu Mkuu ambapo nne zilisema hapana na mbili ziliharibika.
Maalim seif alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kama alivyokuwa makamu
wa mwenyekiti aliyepata kura 653 (aslimia 98.6) ambapo 5 ziliharibika na
4 zilisema hapana.
|