JK azindua kitabu cha Mzee
Kawawa
27/02/2009

JK akimpongeza Mzee Kawawa baada ya kuzindua kitabu chake
Ikulu leo. Kitabu hicho kinachoelezea maisha ya Mzee Kawawa ambaye wengi
wanamwita Simba wa Vita, kimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu chini ya
usimamizi wa Profesa John Magoti, Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere cha
Kivukoni.

JK na rais mstaafu Benjamin William Mkapa wakilonga
wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mzee Kawawa.

Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa na Mh. Pius
Msekwa kwenye uzinduzi huo.

Mama Maria Nyerere akiongea na Rais Mstaafu Benjamin
William Mkapa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mzee Kawawa, Ikulu, Dar
es Salaam.
|