Bidhaa feki za Shilingi
Milioni 25 zachomwa moto
28/02/2009

Maofisa wa kamisheni ya ushindani wa haki (fair
competition commission) wakizichoma moto bidhaa feki zenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 25 kwenye dampo la Pugu Kinyamwezi nje ya jiji
la Dar es Salaam. Msemaji wa kamisheni hiyo amesema bidhaa hizo
zilizoteketezwa zinafanya hesabu ya bidjhaa feki zilizochomwa moto kati
ya mei 2007 na sasa kufikia thamani ya shilingi 1.625 bilioni, amesema
karibu bidhaa zote, ikiwa ni pamoja na balbu, spea za magari, vifaa vya
umeme, feni, waya na kadhalika, ni bidhaa feki ambazo zinatoka China.
|