Waziri Mkuu Mizengo Pinda
atembelea London
03/03/2009

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania,
Mizengo Pinda (aliyekaa watatu kutoka kulia), alikutana na Viongozi wa
Jumuia mbalimbali mjini London katika ziara yake ya kikazi. Alipokelewa
rasmi na Mheshimiwa balozi wa Tanzania nchini UK, Mwanaidi Maajar (aliyekaa
watatu kutoka kushoto). Matembezi hayo yalikuwa kuwashajiisha viongozi
wa jumuia mbalimbali katika jitihada zao za kimaendeleo za jumuia za
Kitanzania zilizopo nchini UK. Kabla ya matembezi ya mjini London,
Mheshimiwa Waziri aliwatembelea jumuia za Northern Ireland.

Mheshimiwa Mizengo Pinda na Mheshimiwa Balozi Mwanaidi
Maajar (Waliokaa) wakiwa
kwenye picha na Maafisa wakuu wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza
ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu alitembelea na kukutana nao kuwapongeza na
kuwashajiisha kwa kazi ya jitihada za kuwahudumia Watanzania nchini UK.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto pichani) akiwalaki
Naibu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini UK, Mh. Ghabaka Kilumanga na
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mh. Mwanaidi Majaar (katikati) nje
ya ubalozi huo Tanzania House mjini London.
|