Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Buriani Mzee Shaaban Khamis Mloo

15/03/2009

Muasisi wa chama cha CUF, Shaaban Khamis Mloo, amefariki dunia jana asubuhi nyumbani kwake mjini Zanzibar. Mazishi yake yalifanyika jana saa 10.00 alasiri huko huko Zanzibar. Marehemu Mzee Mloo alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa chama cha CUF kwa miaka nane, kutoka 1992 hadi 2000 alipochukua nafasi ya umakamo mwenyekiti hadi kustaafu kwake mwaka 2004.

Mzee Shaaban alikuwa miongoni mwa waasisi wa Chama cha CUF kwa kuanzia na vuguvugu la KAMAHURU. Ni yeye ndiye aliyeongoza mazungumzo ya kwanza na wakati huo aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho, James Mapalala, na hatimaye kuungana na kuzaliwa kwa CUF.

Chama hicho kinamtambua Mzee Mloo sio tu kama kiongozi mstaafu wa Chama, bali zaidi kama muasisi au mwanzilishi na alikuwa mwanachama imara na shupavu katika siku zote za uhai wake. Atakumbukwa daima ndani na nje ya chama cha hicho kama mjuzi wa siasa za Tanzania kwa ujumla, mchapakazi na mtu aliyekuwa na ujasiri wa kupigiwa mfano.

Hata baada ya kustaafu umakamo mwenyekiti, Mzee Mloo aliendelea kuwa sehemu muhimu ya CUF kwa kujitolea katika mashauri mbali mbali. Kila alipokuwa na uwezo, hakuacha kuhudhuria mikutano ya hadhara au vikao vyovyote ambavyo alialikwa.

Kikao cha mwisho kuhudhuria ni Mkutano Mkuu wa Nne wa chama cha CUF uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kuanzia 23 hadi 27 Februari, mwaka huu. Kwa hivyo, hadi siku za mwisho mwisho wa uhai wake, Mzee Mloo alisimama imara kuijenga na kuihuisha chama hicho cha CUF.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©