Wakazi wa Kipawa waomba
kusikilizwa
27/03/2009

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Abbas Kandoro (kushoto)
akiwasikiliza wakazi wa kata ya kipawa jijini Dar es Salaam ambao
walimweleza kwamba hawamtaki mkuu wao wa wilaya, Patrick Tsere, kwa
madai kuwa ameshindwa kushughulikia madai yao na kutaka eneo hilo
litangazwe kuwa "janga la kitaifa".
Wakazi hao, ambao waliandamana hadi ofisi za Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege (TAA) zilizo Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere, wanashinikiza kulipwa fidia baada ya kuzuiwa kuendeleza makazi
yao kwa takriban miaka 12 kwa sababu za upanuzi wa uwanja huo.
|