Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mgao wa umeme waanza Dar es Salaam

29/03/2009

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza rasmi mgawo wa nishati ya umeme kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kupungua kwa ufuaji wa umeme kwa megawati 50. Taarifa iliyotolewa leo na Tanesco, ilisema mgawo huo wa muda utakuwa ni wa kila siku kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana na saa 12 jioni hadi saa 4 usiku.

Hali hiyo, taarifa ilisema imechangiwa na kusimama kwa mitambo miwili katika kituo cha Songas (UGT1 na UGT5) ambacho kwa kawaida huzalisha megawati 53. Mmoja unafanyiwa ukarabati wa kawaida na mwingine umeharibika. Ilisema usambazaji umeme kwa Dar es Salaam na Zanzibar unategemea nishati hiyo kutoka mitambo ya nguvu za maji na mtambo wa gesi wa Ubungo kupitia transfoma namba T6 na T7. Pichani juu ni makao makuu ya umeme nchini TANESCO iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

 

 

 

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©