Makuku na Machipsi ya
Muchacho yahamia Upanga
30/03/2009

Chipsi, Kuku na Mishikaki ya Muchacho iliyokuwa
ikipatikana mtaa wa Nyamwezi na Somali sehemu za gerezani jijini Dar es
Salaam, sasa imehamia mtaa wa Mfaume sehemu za Upanga, karibu na
jamatini, njia ya kutokea makao makuu ya Sido.

Hapo mkurugenzi wake Said Muchacho anakwambia mambo ni
mswano ile mbaya na mishikaki sio tu imezidishwa kunoga bali hata ukubwa
na wingi katika spoko zake. Kwa kuwa bwana Said ni mpenzi wa timu ya
Liverpool, ameiita kona yake hiyo Anfield.
|