Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kikwete asema malumbano juu ya Dowans sasa basi

02/04/2009

Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo kwa sababu maalum.

"Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika.

Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete kafikia kudondoa juu ya nguvu ya umeme wa DOWANS katika hotuba yake hiyo baada ya kuona malumbano yasiyokwisha ya chini-chini na kuomba yamalizwe.

Habari zaidi kuhusu uamuzi wa mitambo ya DOWANS bonyeza hapa.

Juhudi hizi za kuleta umeme na huduma bora za umeme kwa wananchi ni moja ya jitihada za Rais Kikwete kutimiza malengo yake tangu alipochukua nafasi ya urais, kwa habari zaidi juu ya mtazamo wa rais juu ya huduma za umeme, rejea habari ya tarehe 21/12/2007 kwa kubonyeza hapa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©