Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

G20 Summit - London 2009

03/04/2009

Tarehe 02/04/2009 waziri mkuu wa UK bwana Gordon Brown alialika wakubwa wa nchi 20 duniani kuhudhuria katika mkutano wa kihistoria ambao mtazamo wake ulikuwa ni kubadilisha mfumo wa uchumi duniani ili kuokoa uchumi ambao hivi sasa upo katika hali mbaya duniani.

Hali mbaya ya uchumi (RECESSION) ambayo imesababishwa na mfumo wa zamani wa kuendesha uchumi duniani, imesababisha nchi nyingi duniani hasa nchi tajiri kukumbwa na hali mbaya ya kiuchumi ikiwemo Marekani na UK.

Bwana Gordon Brown (pichani kushoto) ndie aliyeunda na kupendekeza mfumo mpya wa uchumi kutokana na uzoefu wake katika sekta ya uchumi na ni kama waziri mkuu wa UK. Mfumo huo mpya ulipendekezwa na rais wa Marekani bwana Barack Obama kwa kumpa hongera bwana Gordon Brown kwa juhudi zake za kuunda mfumo mpya wa kuokoa uchumi wa dunia na kuita nchi zote za dunia katika mkutano huu wa kihistoria ambao una mafanikio ya kiuchumi kwa nchi tajiri na kusaidia nchi masikini.

Si Barack Obama tu ambaye alimpongeza Bwana Brown, bali hata marais wengine akiwamo rais wa Ujerumani ambaye alikuwa na wasiwasi wa matokeo ya mkutano huo kabla ya mapendekezo hayo kuwekwa mezani. Rais wa Ujerumani alisifia mapendekezo hayo kwa kusema ni mazuri sana; ambayo yana muelekeo wa kurudisha uchumi wa dunia katika hali yake ilivyokuwa lakini katika mfumo mpya.

Mambo matano muhimu yaliyokubaliwa katika mkutano wa The London Summit 2009 ni kama ifuatavyo:

1. Restoring Confidence, Jobs and Growth: Viongozi wote walifikia kukubaliana katika pendekezo la kukuza uhakika wa kutimiza na kuwajibika katika kukuza imani baina yao viongozi na wananchi wao katika lengo moja la kukuza uchumi kwa kushirikiana pamoja.

2. Strengthening financial supervision and regulation: Viongozi wote walifikia kukubaliana katika pendekezo la kuangalia, kuchunga na kuzirejea kanuni za mfumo mara kwa mara ili kuepukana na kurudia hali mbaya ya uchumi kama ilivyo sasa.

3. Funding and reforming our international financial institutions to overcome this crisis and prevent future ones: Viongozi wote walifikia kukubaliana katika pendekezo la kutoa pesa ambazo zitakuwa kibindoni kwa matumizi ya kusaidia mifuko mbalimbali ya fedha na ya biashara; hasa katika nchi masikini.

4. Promoting global trade and investment and reject protectionism, to underpin prosperity: Viongozi wote walifikia kukubaliana katika pendekezo la kutanua biashara ndani na nje ya nchi kwa kulimbikiza na kuekeza kwa/katika nchi zinazoendelea na kutoa fursa za maendeleo ya nchi zinazoendelea kupata kustawi katika uchumi wa dunia.

5. Ensuring a fair and sustainable recovery for all: Viongozi wote walifikia kukubaliana katika mapendekezo yote hapo juu, kwani uchumi wa dunia unahusu nchi zote tajiri na masikini duniani, kuzipa kisogo nchi masikini kutasababisha kuanguka kwa uchumi wote wa dunia na vilevile kupeana kisogo kwa nchi tajiri kutasababisha kuanguka kwa uchumi wote wa dunia kama ilivyo hivi sasa.

Kwa hivyo, mkutano huu ulikuwa wa kipeke yake na wa kihistoria kwasababu umekusanya mataifa yote kukutana kuwa kitu kimoja kwa lengo moja na kila nchi aidha masikini au tajiri ina fursa ya kustawi na kushirikiana na nchi nyingine ambazo kabla zilikuwa hazina ushirikiano mzuri kwa njia moja au nyingine, lakini angalau kushikana katika njia hii ya uchumi. Bwana Brown alipewa hongera na viongozi mbalimbali kwa mtazamo wake.

Mkutano unaofuata utafanyika New York, Septemba 2009 kuangalia maendeleo yake.

Kuangalia hotuba ya bwana Gordon Brown, bonyeza hapa.

Kuangalia hotuba ya bwana Barack Obama, bonyeza hapa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©