JK mgeni rasmi katika
hafla ya 40 ya Mzee Mloo
07/04/2009

JK akitoa hotuba yake wakati wa kumuombea Dua Marehemu
Mzee Shaaban Khamis Mloo iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada
jijinji Dar es Salaam jioni ya tarehe 04/04/2009. Kulia ni Mwenyekiti wa
Chama Cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba na kushoto ni Katibu Mkuu wa CUF
Maalim Seif Shariff Hamad.

JK akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CUF Profesa
Ibrahim Lipumba na katibu Mkuu wa Chama hicho Seif Shariff Hamad wakati
wa hafla ya kumuombea Dua Marehemu Mzee Shaaban Khamis Mloo ambaye ni
mmoja wa waasisi wa Chama cha CUF. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi
wa hoteli ya Lamada jijinji Dar es Salaam ambapo JK alialikwa kama mgeni
Rasmi.

JK akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha CUF Profesa Ibrahim
Lipumba (kushoto) na Katibu Mkuu wa CUF Seif Shariff Hamad wakitoka nje
ya ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam baada ya
dua ya kumuombea marehemu Mzee Shaaban Khamis Mloo aliyefariki hivi
karibuni. Mzee Shaaban Khamis Mloo alikuwa mmoja wa waasisi wa CUF. Rais
Kikwete alialikwa kuwa mgeni Rasmi katika hafla hiyo.
Kwa vicheko na madaha,
viongozi wa vyama viwili vya Tanzania wamekutana katika tukio ambalo
limeondoa tofauti zao, hiyo ndio Tanzania tunayoijua.
|