Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

KARUME DAY - kumbukumbu za Rais Abeid Amani Karume

08/04/2009

Tarehe 07/04/2009 ilikuwa ni siku ya KARUME DAY ambayo kila mwaka tarehe na mwezi huo hufanyika kumbukumbu ya Rais Abeid Amani Karume. Pichani juu ni ukumbusho wa waasisi wa taifa hili la Tanzania, Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume, walipotembelea Ngome Kongwe huko Zenj enzi hizo. Mwenye kanzu ni Sheikh Thabit Kombo.

Baadhi ya Wananchi wa Zanzibar walohudhuria maombolezi ya Kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar katika kuadhukisha Karume Day.

Viongozi wa Kitaifa akiwemo JK, Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein wakishiriki katika maombolezi ya kumuombea dua njema Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume, katika kaburi lake lililopo nje ya jengo la Ofisi kuu ya CCM, Kiswandui, Zanzibar. Dua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Karume Day ambayo huadhimishwa kila mwaka kumkumbuka na kumuombea kiongozi huyo aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya tarehe 07/04/1972.

Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume (katikati) akiwa pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume (kushoto) pamoja na mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein wakishiriki katika dua ya kumuombea muasisi iliyofanyika katika Kaburi lake lililopo katika jengo la ofisi kuu ya CCM, Kiswandui, Zanzibar.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini walishiriki katika dua ya kumuombea marehemu Abeid Amani Karume katika kaburi la muasisi huyo huko Kisiwandui, Zanzibar.

JK akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, ikulu mjini Zanzibar mara baada ya maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyika Zanzibar tarehe 07/04/2009.

JK akiagana na Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid karume baada ya kuhudhuria shughuli za Karume Day Zanzibar.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©