Dar es Salaam ikitota,
vyenye miguu vinasota
09/04/2009

Dar es Salaam ikitota, vyenye miguu
vinasota, na vile visivyosota vinabakia kukokotwa. Hali hii imekuwapo
kwa muda mrefu sasa na ni hali isiyoridhisha kwa wananchi na wageni au/na
wawekezaji.

Matumbo yakisota viambazani, kupapasa njia
ya kufika nyumbani.

Asie na miguu minne hukimbilia viambazani,
hawezi kukwepa mawimbi kama aliye kisiwani.

Asubuhi hugeuka kuwa jioni, na
pakukanyagia hupaoni.

Mitaa hugeuka kuwa mito, vyenye kusota
vinaelekea kingoto.

Vyote vinavyokwenda vinasota, kuanzia
Vespa mpaka Toyota.
Lakini hii ni ishara nzuri ya kuonyesha
mifano hai ambayo inahitaji kufanyiwa kazi kwa malengo ya maendeleo ya
nchi kwa miaka inayokuja kama sio miezi.
|