Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Bi Salma mgeni wa heshima SACOSS - Zanzibar

13/04/2009

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mweka hazina wa SACCOS ya Meli Nne, Bi Shamsa Saleh Hilal, mchango wa Shilingi Milioni Tano 5m/- kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa SACCOS uliofanyika katika Chuo cha Karume, Mwanakwerekwe, Zanzibar. Kulia ni Waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.

Baadhi ya Wanachama wa SACCOS Ya Meli Nne jimbo la Mwanakwerekwe, Zanzibar wakimshangalia Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia huko Chuo cha Karume, Zanzibar. Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Tatu pamoja na viongozi wa SACCOS hiyo.

Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Meli Nne Mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa SACCOS hiyo huko Mwanakwerekwe, Zanzibar. Katika Hafla hiyo Mama Kikwete aliahidi kuichangia shilingi Milioni Mbili na nusu 2.5m/-.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©