Uji wa tope Jangwani, Dar
es Salaam
23/04/2009

Picha hizi
zimepigwa na mpita njia na kuleta rai zake kama ifuatavyo.
"Njia hii inayokatisha
viwanja vya jangwani inahitaji ubunifu kidogo tu kuelewa kwamba endapo
itatengenezwa itasaidia sana foleni katikati ya jiji, ukizingatia dereva
pichani akitaka kwenda maeneo ya Kigogo ama Ilala akitokea sehemu za
faya iwapo barabara hii ingekuwa safi na nzuri, dereva hana haja ya
kupita barabara ya shule ya Uhuru...

ama anayetoka Magomeni au
Mwananyamala na anataka kwenda sehemu za Ilala ama Temeke hana haja ya
kuzunguka barabara za Kawawa Road ama Morogoro Road...

tutumai kwamba Mh. William
Lukuvi atafanya utaratibu juu ya swala hili".
|