Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ubunifu wa usanii wa picha za 3D

26/04/2009

Ubunifu wa usanii wa picha za uchoraji wa aina ya pembe tatu au 3D umechukua hatua ya pili kwa wenye kipaji cha uchoraji wa picha hizo.

Ubunifu huu wa kuchora milango, magari na kuta za nyumba unachukua hatua kubwa na unakuja kwa mwendo wa kasi na kukuzwa na kipaji cha bwana Thomas Sassenbach ambaye anafanya biashara ya uchoraji huo.

 

Uchoraji wa picha za 3D zinakuwa na hisia ya kuona kitu kama kweli kipo mbele yako hai, wakati kitu hiko si hai bali ni ya kuchorwa kama ionekanavyo ndege hiyo hapo pichani.

Picha ya karibu ya ndege aina ya Supersonic Jet ambayo wateja wengi wa bwana Thomas huipendelea kuichagua kuchorewa kwenye sehemu zao za kinyumba na kibiashara.

Picha za milango ya gereji (garage) huleta sura ya vitu kuonekana kama vitu hai kama inavyoonekana gari ya mashindano ya Formula One pichani.

Hii ni picha ya mtu mwingine ambaye kachorewa picha ya gari ya Formula One.

Picha hii inaonekana kama ni mlango wa kuendea baharini.

Bwana Thomas ni mtu wa kutoka mji wa Munich, Germany, na wateja wake hutoka nchi mbalimbali duniani kwa kazi ya uchoraji wake wa 3D.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©