Kikwete aomboleza kifo cha
Aisha Adam Sapi
27/04/2009

JK akiwafariji ndugu na
jamaa wa Marehemu bibi Aisha Adam Sapi Mkwawa wakati Rais alipokwenda
kuwapa pole kufuatia kifo cha mke huyo wa spika wa Zamani wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

JK akiweka saini kitabu
cha Maombolezo nyumbani kwa marehemu bibi Aisha Adam Sapi Mkwawa wakati
Rais Kikwete alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho na kuwafariji
ndugu wa Marehemu. Bibi Aisha alikuwa mke wa Marehemu Adam Sapi Mkwawa
aliyekuwa spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwili wa Bibi Aisha ulisafirishwa baadaye kwenda Iringa kwa Mazishi.
|