Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

$2.4 Milioni kuipendezesha Forodhani

28/04/2009

Bustani ya Forodhani, Zanzibar (Forodhani Park) imerudishwa katika hali yake kama ilivyokuwa wakati huo wa Sultan wa Zanzibar kwa msaada maalum wa Aga Khan Trust for Culture (AKTC) kwa gharama ya dola 2.4m. Forodhani ni sehemu ambayo hupendwa kutembelewa na wengi ambao ni wakazi wa Zanzibar na wageni wanaotembelea Zanzibar. Ni sehemu mojawapo ya kivutio cha matembezi ya Zanzibar.

Hii ndio ilivyokuwa bustani ya Forodhani kabla ya matengenezo mapya.

Moja ya nyumba ambazo zimepata kurejeshwa hali yake iliyokuwa kama zamani ni nyumba iliyo pichani (The Old Dispensary).

The Old Dispensary ikionekana pichani baada ya kufanyiwa ukarabati wa nguvu na mradi maalum wa Aga Khan Trust for Culture. The Old Dispensary sasa imepewa jina jipya na sasa inajulikana kama The Stone Town Cultural Centre.

Bonyeza kwenye mchoro wa Forodhani Park kwa kuona sehemu zilizoainishwa ambazo zinafanyiwa ukarabati na kurudishwa hali yake kama ilivyokuwa zamani.

Zanzibar ina nyumba nzuri za ajabu na za kihistoria ambazo zina-akisi utamaduni wa Zanzibar na ufahari wa Tanzania nzima. Msaada wa Aga Khan Trust for Culture (AKTC) umesaidia kuhifadhi nyumba na sehemu zenye kihistoria Zanzibar na hii ni moja ya mfano wa kusaidia utamaduni wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa ujumla kutokupotea.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©