Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Sherehe za Muungano London

29/04/2009

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mama Mwanaidi Senare Maajar, pamoja na Baba Balozi, Bwana Sherif Maajar, waliwakaribisha Mh. Dr Lindiwe Mabuza, Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Uingereza, akifuatiwa na Balozi wa Msumbiji, Mh. Antonio Gumede.

Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar pamoja na Baba Balozi, wakimkaribisha Balozi wa Botswana na vilevile ni Mkubwa wa Mabalozi wa Nchi za Afrika hapa Uingereza, Mh. Roy Blackbeard.

Mabalozi, Wawakilishi, Wanajumuiya za Watanzania na baadhi ya Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba iliyotolewa na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, kwenye hafla ya Muungano iliyofanyika Ubalozini, London.

Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania kwenye Sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Toka kulia ni Bwana Abubakar Faraj, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana Katega, Muwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, Bwana Maina, Mwenyekiti wa chama cha CCM Reading, Bwana Jackson, Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, na Bwana Fredy (nyuma ya picha) Mtanzania na Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London.

Mheshimiwa Balozi, akiwa nje ya Westminster Abbey, London na Maofisa wengine wa Ubalozi, baada ya kumalizika hafla ya Muungano ambayo huandaliwa kwa Kila Nchi Mwanachama wa Commonwealth (mojawapo ni Tanzania) zinapofika siku kuu za nchi za Mataifa ya Commonwealth. Kulia mwa picha ni Bwana David Nginilla, Bwana Amos Msanjila, Mh. Balozi, Mama Mwanaidi. S. Maajar, Dada Caroline Chipeta, na Bwana Clement Kiondo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©