Mbagala na Majeruhi wa
mabomu watembelewa
01/05/2009

Kikwete akiangali baadhi
ya vipande na mabaki ya mabomu vilivyookotwa katika makazi ya watu
wanaoishi karibu na kambi ya Jeshi la wananchi Mbagala jijini Dar es
Salaam ambapo nyumba kadhaa ziliharibiwa vibaya na kwa mujibu wa taarifa
ya polisi watu sita kupoteza maisha na 236 kujeruhiwa wakati ajali
ilipotokea katika ghala la kuhifadhia silaha za kivita katika kambi hiyo.
Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa usalama na utambuzi
Jeshini Brigedia Jenerali Paul Meela, Naibu Waziri wa Ulinzi na jeshi la
kujenga Taifa Emanuel Nchimbi, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama
Jenerali Davis Mwamunyange na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said
Mwema.

Makamu wa Rais Dk Ali
Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la
Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali F. N. Ulomi, wakati
alipotembelea Kambi ya Jeshi hilo eneo la Mbagala ambapo milipuko ya
mabomu ilitokea jana na kusababisha madhara makubwa ya mali na watu.

Rais Kikwete akimpa pole
mtoto Mariam Is-haq (8) aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke
baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali iliyotokea katika
ghala la kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi huko Mbagala jijini Dar
es Salaam. Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Suleiman
mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar es Salaam.

Madaktari Bingwa katika
Taasisi ya Mifupa ya Moi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbil(kulia)
wakimpa Rais Kikwete (kushoto aliyevaa mavazi maalum) maelezo ya mgonjwa
aliyejeruhiwa vibaya na moja ya mabomu yaliyolipuka katika ajali
iliyotokea katika ghala la kuhifadhia zana za kivita katika kambi ya
jeshi la Wananchi wa Tanzania huko Mbagala, jijinji Dar es Salaam.
Mgonjwa huyo amepoteza mguu wa kulia na amepoteza damu nyingi na
anapumua kwa kutumia mashine maalum (Life Supporting Machine ). JK alirejea
jijini Dar es Salaam akitokea mjini Arusha ambapo alihudhuria mkutano wa
wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwenda huko moja kwa
moja.
|