Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Polisi wapambana na majambazi Dar es Salaam

08/05/2009

Mpambano kati ya Polisi na majambazi waliovamia mtaa wa Swahili ulimalizika na miili ya majambazi watatu kuuliwa hapo hapo na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.

Majambazi hao ambao wakati walipokuwa wakirushiana risasi na Polisi, walikuwa wamebana karibu na gari iliopo kulia chini (pichani). mmoja wao alikuwa amevaa mkanda wa risasi na alikuwa anamwaga njugu kama hana akili vizuri.

Wakati wa mpambano huo, baadhi ya watu walithubutu kutoa pua wasipitwe na tukio la roho mkononi.

Mtaa wa Swahili ulikuwa katika hali ya heka heka.

Raia na Polisi walikuwa makini na nafsi zao wakati wa pambano hilo.

Lakini kila kitu kina mwisho wake. Mmoja wa majambazi waliouwawa akionekana akitiwa nyuma ya gari la Polisi.

Heka heka hizo zilidumu kama dakika 45 mpaka Polisi kufikia kushinda.

Gari mojawapo ambayo inashukiwa ilikuwa ya majambazi ikikaguliwa vilivyo na huku FFU wakiangalia kwa makini kabisa.

Askari wote wake kwa waume walikuwa na kifaa, kuanzia bastola, bunduki, mabomu ya machozi, n.k.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©