UK yasaidia walioathirika
na mabomu ya Mbagala
15/05/2009

Mkuu wa
idara ya maendeleo ya kimataifa wa Uingereza nchini Tanzania, bwana
Darren Welch, akitoa msaada wa vifaa vya shule ya msingi ya Mbagala Kuu
kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana Paul Daniel, ikiwa moja ya mchango
wa walioathirika na mabomu yaliyolipuka Mbagala, Dar es Salaam.
United
Kingdom kupitia idara yake maalum iliyopo nchini Tanzania (DFID)
Department for International Development, imetoa $90,000 (takriban Tsh.
122 milioni) kwa kutoa msaada wa haraka sana kwa waliofikwa na maafa ya
mlipuko wa mabomu ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
|