Obama ahimiza kufungwa kwa
Guantamo Bay
22/05/2009

Rais wa Marekani, Barack Obama, katika
hotuba aliyotoa mjini Washington ameutetea mpango wake wa kutaka
kuifunga jela ya Guantamo Bay kisiwani Cuba.
Obama alisema kuwa kuimarisha jela ya
Guantamo Bay, imedhoofisha usalama wa taifa la Marekani (National
Security).
Kwa mujibu wa mpango wa Obama, baadhi ya
wafungwa 240 waliokuwepo Guantamo Bay, iliyopo Cuba, wahamishiwe
Marekani katika jela zilizo na ulinzi mkali, baadhi yao watashtakiwa
mahakamani Marekani, wengine watafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi
na wengine wataachiwa huru kuambatana na amri zilizotolewa na mahakama.
Hapo awali, Obama alikataliwa kisiasa na
Seneti kupewa dola milioni 80 kwa ajili ya mpango wa kuifunga jela ya
Guantamo Bay.
|