Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mufti Simba asafiri kukaguliwa Afya yake

24/05/2009

Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaban Simba, ameondoka nchini kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa waandishi wa habari zinasema kuwa, Mufti Simba ameondoka na kaimu katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Said.

Habari za kusafiri kwa Mufti zilithibitishwa pia na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-hajj Mussa Salum, alipozungumza na waandishi wa habari.

Mufti amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya shinikizo la damu na kisukari kwa muda mrefu na mara kadhaa amekuwa akisafiri kwenda India kwa uangalizi wa afya yake.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©