Polisi ashambuliwa na
Wanajeshi
25/05/2009

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es
Salaam limesema, bado halijakabidhiwa ripoti ya tukio la Wanajeshi
waliomshambuliwa askari wake wa kikosi cha usalama barabarani, Thomas
Mayapila wiki iliyopita wakati akiongoza magari katika mitaa ya Ubungo.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo,
Evarist Mangalla alisema bado hawajakadhiwa ripoti hiyo.
Mangalla alisema wanaendelea kuisubiri
ripoti ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja kwa yule
atakayebainika kuwa na makosa.
Baada ya tukio hilo ambalo lilidaiwa
kuhusisha askari zaidi ya mmoja, iliundwa timu ya askari ya Polisi na
JWTZA ili kuanza uchunguzi huo.
|