Jumuia mpya ya Watanzania
UAE
06/06/2009

Balozi
wa Tanzania nchini UAE, Mohamed Maharage Juma akimpongeza Mwenyekiti
mpya wa jumuia ya Watanzania ambayo imeanzishwa na Watanzania nchini UAE,
Bw Mohamed Shariff (kulia) na katikati ni Consul General, Ali Ahmed
Saleh.

Mgeni wa
heshima Mhe. Mohamed Maharage Juma, Balozi wa Tanzania nchini UAE (Umoja
wa Falme za Kiarabu) aliyeongozana na Bw. Ali Ahmed Saleh Consul General
wa Tanzania Dubai na Emirate za Kaskazini za UAE wakiwa pamoja na baadhi
ya viongozi wapya wa jumuia mpya ya Watanzania (TAE) iliyozinduliwa
nchini UAE. Mhe Balozi aliupongeza uongozi uliomaliza muda wake kwa kazi
nzuri walioifanya ya kuasisi Jumuia na kuifikisha ilipo sasa na kuupa
chanagamoto uongozi mpya kufanikisha malengo ya Jumuia na akaahidi
kwamba Ofisi za Ubalozi na Consulate zitaendelea kusaidia shughuli za
Jumuia kwa kadri ya uwezo wake.

Baada ya mkutano,
Watanzania wanaoishi UAE walijumuika kupata mlo wa pamoja.
Viongozi Wakuu
wapya ni kama wafuatao:
-Bw.
Mohamed Shariff (Mwenyekiti)
-Bw.
Mbarak Ahmed (Naibu Mwenyekiti)
-Bw.
Shabir Damji (Katibu Mkuu)
-Eng.
Issa Majid Magdi (Naibu Katibu Mkuu)
-Bw.
Mohamed Manji (Mweka Hazina)
-Bw.
Hassan Ally Abri (Naibu Mweka Hazina)
-Bw
Abdulrahman Hassan (Mkurugenzi, Kurugenzi ya Jamii na Vijana)
-Bi
Rahma Bukheti (Mkurugenzi Kurugenzi ya Wanawake)
-Bw
Isaac Peter (Mkurugenzi Kurugenzi ya Mawasilano na Uhusiano)
|