KNIGHTS kukuza mfuko wa
watoto walemavu
11/06/2009

The Knights Charity wamefanikisha tamasha
la michezo ambayo imefanyika katika viwanja vya Kijitonyama, Dar es
Salaam, kwa dhumuni la kukuza mfuko kwa watoto walemavu kusaidia Jeshi
la Uokovu (Salvation Army) ambao wanaangalia watoto hao walemavu.

Michezo mbalimbali iliandaliwa katika
tamasha hilo ikiwamo 'Knight Rider, Dragons Smoky Lair, Lance-A-Lot,
Chariots of Fire na Excalibur'

Wahudumu (waiters) walitumia baiskeli
kuhudumia waliofika katika viwanja hivyo.

Washindi wa michezo hiyo siku hiyo
waliondoka na zawadi kem kem.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Lawrence
Masha alikuwa ni mmoja wa waalikwa na mmoja wa walioshiriki michezo hiyo.
Timu yake ilishinda mchezo wa Wanazimamoto (Fire Fighting Drill).
|