Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kikwete aonya Mafisadi

12/06/2009

Katika mtikisiko wa uchumi duniani, Serikali imetangaza kutenga shilingi trilioni 1.7 za mpango wa kupunguza mzigo kwa wananchi wake kutokana na hali ya msukosuko wa kiuchumi, Rais Jakaya Kikwete ameonya kuwa yeyote atakayejaribu kujihusisha na ujanja ujanja wa kutaka kujitwalia fedha hizo kwa manufaa binafsi atashughulikiwa ipasavyo.

Rais ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wabunge, wazee na wananchi wa mkoa wa Dodoma kuhusu hali ya uchumi nchini.

Amesema Serikali imepanga kutumia kiasi hicho cha shilingi trilioni 1.7 katika bajeti yake ya mwaka mpya wa fedha na hivyo ni lazima zitumike kwa malengo yaliyowekwa na si vinginevyo.

Akizungumzia kuhusu sekta mbalimbali zinazoguswa na mpango huo, Rais Kikwete amesema, Serikali italipa fidia vyama vya ushirika na makampuni yaliyonunua mazao na kushindwa kuwalipa wakulima.

"Hatutalipa madeni ya zamani... na nitumie fursa hii kuwaonya watu wanaopanga mikakati ya kujichomeka kiujanja ujanja ili watafune fedha kwa maslahi yao binafsi," akasema.

Amesema msukosuko huo wa uchumi ni wa muda na hivyo changamoto zilizopo ni kutafakari jinsi ya kujinusuru na nini kifanyike ili kubadili uelekeo.

"Ni imani yetu kuwa msukosuko huu ni wa muda tu kwa kuwa umeshawahi kutokea miaka ya nyuma na ukapita kiasi kwamba uchumi wa dunia ukakua zaidi," amesema.

Ili kukabiliana na hali hiyo mikakati mbalimbali iliyowekwa na Serikali ni kulinda ajira katika sekta mbalimbali na kuhakikisha upatikanaji wa chakula.

Kadhalika kulinda sekta ya uwekezaji na kulinda mahitaji muhimu ya kijamii ikiwa ni pamoja na afya na elimu.

Hotuba hiyo ya Rais Kikwete aliyoitoa kwa zaidi ya saa moja katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©