Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Madhehebu ya dini yapinga kuondoshwa misamaha ya kodi

16/06/2009

SERIKALI inajitahidi katika mbio za UCHUMI NA KUSAIDIA JAMII nchini. Pamoja na kuwa uchumi mwaka 2008 umeongezeka kwa asilimia 6.4 kwenye sekta ya uwekezaji wa mitaji ya kigeni peke yake, serikali zinazungusha pesa hizo katika maeneo mbalimbali ya kuendeleza nchi ikiwemo maeneo ya kusaidia jamii.

Lakini baadhi ya jumuia za NGOs na madhehebu ya dini ambao wanatoa baadhi ya huduma kwa jamii wamesikitishwa na wamepinga vikali matokeo ya bajeti ya Mwaka 2009/2010 ambayo imefuta misamaha ya kodi (VAT) kwa jumuia za NGOs na jumuia za Kidini ambazo hapo awali jumuia hizo zilisamehewa kodi zake za VAT kwa kuwapa mwanya jumuia hizo kutoa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali na kupunguzia baadhi ya mizigo ya serikali.

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, amesema Kanisa limesikitishwa na kusononeshwa mno na bajeti hiyo kwa vile inakatisha tamaa taasisi za kidini ambazo zinatoa huduma njema, hususan makanisa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©