Dk. Shein kuaga mwili wa
Omar Bongo - Gabon
17/06/2009

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein
akitia saini kitabu cha maombolezo Ikulu mjini Libreville, nchini Gabon
kufuatia kifo cha Rais wa Nchi hiyo Marehemu Omar Bongo kilichotokea
tarehe 8 Juni 2009 mjini Barcelona Hispania alikokuwa akitibiwa.
Marehemu Bongo anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Nchini Gabon.

Askari wa Jeshi la Gabon wakisindikiza
Jeneza lenye mwili wa Rais wa Gabon marehemu Omar Bongo aliyefariki
Dunia tarehe 8 Juni 2009 nchini Hispania alikokuwa akitibiwa kuelekea
uwanja wa ndege wa Nchi hiyo ulipokua ukitokea Ikulu mjini Libreville
ukipelekwa kijijini kwake kwa maziko.
|