Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Hitma kwa waliokufa ajali ya meli Zanzibar

21/06/2009

Uongozi wa kampuni ya meli ya Fatih Express umeandaa hitma ya kuwaombea watu sita waliopoteza maisha katika ajali ya meli hiyo iliyotokea hivi karibuni katika bandari ya Zanzibar.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Said Abdulrahman Juma alisema kuwa, hitma hiyo itafanyika katika msikiti wa Ijumaa wa Malindi baada ya swala ya Alasiri na itahudhuriwa na wananchi mbalimbali wakiwamo na masheikh mbalimbali.

“Tumeamua kufanya hitma kwa ajili ya ndugu zetu, sisi tumeguswa sana na maafa hayo, hivyo tunaomba wananchi wote wanaoweza kuhudhuria wafanye hivyo ili tuwaombee wenzetu” alisema Juma.

Habari za ziada, idara za mamlaka ya bandari zikishirikiana na timu ya waopoaji wa meli hiyo iliyozama katika bandari ya Malindi, Zanzibar Mei 29, 2009, ilionywa na Nahodha wa meli hiyo bwana Usi Ali Usi katika uopoaji huo kuwa jitihada za kuopoa meli hiyo zisipofanywa kwa umakini, zinaweza kusababisha uchunguzi wa ajali hiyo kutokwenda sawa.

Nahodha Usi Ali Usi alizungumza na waandishi wa habari kwa mara yake ya kwanza tangu kutokea ajali hiyo alisema, taarifa kuwa meli hiyo inamomonyoka kutokana na kuchakaa wakati wa kuvutwa si wa kweli.

Alisema tatizo ni watu kutofunga minyororo katika sehemu ngumu za meli zilizowekwa maalum kwa kazi hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©