Serikali yafuta ushuru kwa
madhehebu yote ya Dini
24/06/2009

Wiki moja baada ya serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania kutangaza kuanza kutoza ushuru kwa mashirika yote
ya Dini wakati ikiwasilisha bajeti ya Mwaka 2009/10 bungeni mjini Dodoma
na kuzua maswali mengi kutoka kwa Wabunge.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda ametangaza rasmi
kufuta ushuru Kwa madhehebu yote ya Dini na kurejea kama Mwanzo.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amewakilisha kwa kutangaza uamuzi huo mjini
Dodoma.
|