Nasma Khamis afariki dunia
25/06/2009

FANI ya muziki wa taarabu nchini imepatwa
na msiba wa kufariki mtunzi na mwimbaji mahiri, Nasma Khamis, umaarufu
wake 'Kidogo'.
Nasma, 57, ambaye anakumbukwa kwa baadhi
ya nyimbo zikiwamo, Mtu Mzima Ovyo, alifariki juzi jijini Dar es Salaam.
Kulingana na ndugu zake, Nasma alifariki
saa sita usiku kwenye Hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa kutokana na
kusumbuliwa na malaria.
Baba mdogo wa marehemu, Hamis Mohamed 'Kaniki'
aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake Kinondoni, Dar es Salaam
ambako kumewekwa msiba huo kuwa Nasma alikuwa akisumbuliwa na shinikizo
la damu mara kwa mara, lakini wiki iliyopita alilazimika kulazwa Temeke
kutokana na hali yake kuwa mbaya na uchunguzi ulionyesha pia alikuwa na
malaria.
|