Michael Jackson afariki
dunia
26/06/2009

Michael Jackson, bingwa wa pop duniani
amefariki dunia kwa kinachosadikiwa kuwa mshtuko wa moyo.
Michael Jackson amefariki akiwa na umri wa
miaka 50. Mfanyakazi wa nyumbani kwake aliita 'Ambulance' kumuwahisha
hospitali ambapo inasemekana hakuweza kuzinduka.
Michael Jackson ameacha watoto watatu.

Michael Jackson akiwa na rais mstaafu,
Al-hajj Ali Hassan Mwinyi alipotembelea Tanzania miaka ya 90.

Pichani juu akipokelewa uwanja wa ndege wa
Tanzania katika miaka ya 90 na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati
huo, Hayati Diria.

Michael Jackson ni mmoja
wa wanamuziki wachache kukaribishwa Ikulu ya marekani ya White House kwa
mchango wake katika muziki nchini Marekani katika miaka ya 80. Kulia kwa
Michael ni aliyekuwa rais wa Marekani, Ronald Reagan na kushoto kwa
Michael ni mke wa rais Reagan, Nancy Reagan.
|