Kaimu Mufti Mkuu Sheikh
Suleiman Gorogosi afariki ajalini
27/06/2009

Kaimu
Mufti Mkuu, Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki dunia katika ajali ya
gari akiwa safarini akitokea Mtwara kwenda Lindi.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana marehemu Gorogosi aliondoka Dar es
Salaam kwa ndege kwenda Lindi kupitia Mtwara, akashuka na ndege mtwara
kuelekea Lindi na gari ambapo inasemekana tairi la mbele la gari
alilokuwa akisafiria lilipasuka na gari kupinduka.
|