Rubani afia angani
03/07/2009

Ndege ya
Continental ikitokea Brussels kwenda New York ilibidi leo litue kwa
dharura katika uwanja wa ndege wa Newark baada ya rubani kufariki dunia
wakati wakiwa angani.
Ndege
hiyo aina ya Boeing 777, ikiwa na abiria 247 ilitua salama mnamo saa
kumi katika uwanja wa New Jersey, ambao ni mmoja kati ya viwanja vitatu
vya jiji la New York.
Shirika la ndege la Continental
katika taarifa yake limesema rubani huyo alikuwa na umri wa miaka 61
akiishi mjini Newark na alishafanya kazi kwa muda wa miaka 21. Hadi sasa
sababu ya kifo cha rubani huyo haijajulikana.
Shirika
la ndege la Continental ni la tano kwa ukubwa duniani na hutoa huduma
kati ya Brussels na New York-Newark kila siku, na kuhudumia njia
zipatazo 230 za Marekani, Latin na Amerika ya Kusini pamoja na
Caribbean.
|