Maonyesho ya Sabasaba 2009
06/07/2009

Maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu (2009)
yamepiga hatua na sio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mandhari na
majumba ya walioshiriki katika maonyesho hayo yametengenezwa kileo na
hata milango ya kuingilia Sabasaba (pichani juu) imetengenezwa kileo na
ya kupendeza na sio kama ilivyokuwa zamani.

Lango
kuu la kuingilia kwenye maonyesho ya sabasaba ya mwaka 2009.

Vodacom
Tanzania wamejipanga kisawasawa mwaka huu na harakati mbalimbali.

Sura
mpya za aina ya mabanda zinaonekana safari hii.

Wachina
ambao wana historia ya kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba tangu enzi
na enzi, mwaka huu wamechukua mtaa mzima kuonyesha hatua waliopiga ya
uzalishaji.

Watani
wa jadi na wao wako kamili kabisa.

Banda la
wizara ya utalii na maliasili nao waliweka vitu vyote kuvutia watalii.

Njia ya kuelekea bustani ya wanyama pori
ndani ya banda la wizara ya maliasili na utalii.

Inapendeza kwa wale ambao hawajapata kuona
mali asili zao, wanapata muamko wa kuona mali asili ya nchi yao wakiwa
jijini Dar es Salaam kwa njia ya usalama kabisa.

Watu mbalimbali wakiwa ndani ya bustani ya
wanyama, wakimshangaa chatu mkubwa huku wakipewa maelezo mbalimbali
kuhusiana na nyoka huyo mkubwa.

Pundamilia, moja ya wanyama wetu
tunaojivunia nao Watanzania.

Sehemu ya mito asilia ikionyeshwa kwenye
sehemu maalum iliyotengewa.

Sehemu ya shamba iliotegwa mizinga ya
nyuki.

Pichani ni bustani ya miche ya miti ambayo
ilitengewa sehemu yake maalum ya kuonyeshwa kwa waliozuru katika
maonyesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2009.
Maonyesho ya Sabasaba hutokea kila mwaka
kuanzia tarehe 1 Julai mpaka kuadhimishwa kwake tarehe 7 Julai katika
viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, Kilwa Road, Dar es Salaam, Tanzania.
|