Kikwete acharuka, ataka
Mabilioni yake yarejeshwe
08/07/2009

RAIS Jakaya Kikwete ametaka kurejeshwa kwa
fedha alizozitoa kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wananchi kuinua
vipato vyao maarufu kama 'Mabilioni ya Kikwete' kama hazijafanyiwa kazi
kama iliyokusudiwa.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete alitoa wakati
alipotembelea maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa (BET) kwenye
viwanja vya maonyesho vya kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Kikwete alisema uamuzi huo unatokana na
kutofanyiwa kazi kwa fedha hizo kama ilivyokusudiwa jambo ambalo
analiamini kutokana na wananchi wake kulalamika.
"Fedha hizo ni zangu kama mmeshindwa
kuzizungusha kwa wananchi naomba mzirudishe kwa kuwa nilizitoa kwa nia
ya kuwasaidia wananchi wangu ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya
maisha," alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa lengo la kutoa fedha hizo
ni kuwasaidia wananchi wake na kuleta tija kwa maendeleo ya nchi na sio
watu wachache jambo ambalo limekwenda kinyume na utaratibu.
|