Hitma ya Sheikh Gorogosi -
Dar es Salaam
09/07/2009

JK
akisalimiana na baadhi ya waumini walioshiriki katika Hitma maalumu ya
kumuombea Marehemu Sheikh Suleiman Gorogosi iliyofanyika katika Msikiti
wa BAKWATA, Kinondoni Muslim.

JK
akiteta jambo na Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban bin Simba, pamoja na
Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam, Al-hajj Musa Salum, wakati wa Hitma ya
kumuombea marehemu Sheikh Suleiman Gorogosi aliyefariki hivi karibuni
kwa ajali ya gari huko Lindi. Hitma hii ilifanyika katika msikiti wa
BAKWATA Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam. Mufti Mkuu (pichani
kushoto) inabidi akae kitini kutokana na sababu za kiafya.
|