Balozi Mohammed Maharage
atoa Shukrani
12/07/2009

Familia ya balozi wa Tanzania nchini UAE
bwana Mohammed Maharage Juma, inachukua fursa kuwashukuru wote ambao
walioweza kushiriki katika mazishi na kuifariji familia kwa kufiwa na
binti yao mpendwa Fatuai binti Mohammed aliyefariki Julai 08, 2009 na
kuzikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam.

Rais
Mstaafu Mh. Benjamin William Mkapa akimfariji Balozi Mohamed Maharage
Juma baada ya mazishi ya bintiye katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es
Salaam. Kati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mheshimiwa Bernard Membe.
|