MICHUZI amzawadia mgeni wa
Milioni 6
16/07/2009

Kaka
Issa Michuzi (pichani kulia) akimpongeza Lugazo Semdili (kushoto pichani),
mume wa mgeni wa Milioni 6 wa Globu ya Jamii (Michuzi Blogspot), Fatma
Shefa, aliyempokelea mkewe zawadi ya dola 1000 kupitia huduma ya M-Pesa
ambayo inatolewa na kampuni ya simu ya Vodacom.

Kaka
Michuzi akimshukuru Rukia Mtingwa wa Vodacom baada ya kampuni hiyo
inayoongoza ya simu za mkononi kutimiza ahadi yake ya kumdhamini mgeni
wa milioni 6 kwa kumzawadia dola 1000.

Mgeni wa
Millioni 6 wa Globu ya Jamii, Fatuma Shefa, anayesoma katika Chuo Kikuu
cha Coventry University, Uingereza, hatimaye amekabidhiwa kitita chake
cha dola 1000 kupitia huduma makini ya M-Pesa ya Vodacom baada ya mgeni
huyo kuzuru Globu ya Jamii ya Michuzi Blogspot akiwa kama mtu wa milioni
6.
|