Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Maonyesho ya historia ya Soka (Soccer) nchini Tanzania

23/07/2009

Sehemu ya majengo mapya ya makumbusho na nyumba ya utamaduni Dar es Salaam (ndipo palipofanyika maonyesho ya historia ya soka nchini) zamani ikijulikana kama makumbusho ya taifa, ambayo inafanyiwa ujenzi pamoja na ukarabati wa nguvu kazi ambayo inategemewa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu na kupafanya mahali hapa sio tu pa kutunzia historia bali pia sehemu ya kukutana na kuburudika kwa tafrija mbalimbali na vyakula vya asili na mengineyo.

Tangazo la onesho la kumbukumbu ya soka nchini ambalo tarehe zake zimesogezwa mbele kwa mwezi mzima kutokana na maombi ya wahudhuriaji na wapenzi wa soka.

Mtaalamu wa utafiti na mtunza historia katika makumbusho na nyumba ya utamaduni B. Margreth M. Mapunda akionesha kitabu chenye historia ya mpira wa miguu ambacho amekiandaa kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu hiyo muhimu. Kitabu hicho kinapatikana hapo makumbusho na nyumba ya utamaduni na kina historia ndefu tokea enzi za Sunlight na Gossage cup, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa enzi hizo pamoja na viongozi.

Mmoja wa waliohudhuria maonesho hayo akiangalia jezi namba 3 mgongoni iliyovaliwa na beki hatari wa Taifa Stars enzi hizo Mohamed Chuma wa Mtwara aliyovaa siku anastaafu kuchezea timu ya taifa mwaka 1976.

Mhudhuriaji wa maonesho ya historia ya soka akiangalia nyota wa zamani wa soka nchini.

Sehemu ya ukumbi wa maonesho wa makumbusho na nyumba ya utamaduni.

Wachezaji wa jimbo la nyanda za juu kusini mwaka 1955 katika kombe la Sunlight, uwanja wa Ilala, siku hizi uwanja huo unajulikana kama uwanja wa kumbukumbu ya Karume.

Viongozi wetu walikuwa wapenzi wakubwa wa michezo. Simba wa vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa akiiingia uwanjani kama refa katika mechi ya wabunge na mabalozi miaka ya 70.

Mwalimu Julius Nyerere akiwa na wachezaji na viongozi wa timu ya taifa aliowakaribisha Ikulu baada ya kunyakua kombe la Gossage cup mwaka 1964.

Nahodha wa timu ya taifa Mbwana Abushiri (Director Mbwana) akiwa kabebwa juu na wenzie baada ya kunyakua kombe la Gossage cup mwaka 1964.

Timu ya taifa wakiwa na kocha wao Millan Celebic (shoto juu) mwaka 1965.

Baadhi ya marefa waandamizi miaka ya 1970 akiwemo Manyotto Ndimbo (wa sita kulia) na Rajabu Marijani (wa nane kulia).

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©