Kijana mrefu kuliko wote
Tanzania
28/07/2009

Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote
Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu
kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana
jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini
aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka
mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga
mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka
kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi
(Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje
ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake
kamili na anafanya nini. Inasemekana kuna watu wanamfuatilia kumsaidia
umaarufu.
|