Tahadhari ya Majambazi
30/07/2009

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Afande Suleiman Kova alitoa tahadhari na kuwataka wote
wanaohusika kukaa makini kuwa kuna kundi kubwa la majambazi wenye silaha
kali, ambao wameingia Jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Wahalifu hao ni pamoja na Wakenya ambao
wana tabia ya kupora fedha katika taasisi kubwa kama mabenki, kampuni za
mafuta na sehemu zenye biashara kubwa n.k.
Aliendelea kutoa onyo kamanda Kova na
kusisitiza, watu hawa wana mbinu ya kula njama na watumishi wasiokuwa
waaminifu. Ni muhimu mkafuatilia mienendo mbalimbali katika benki zenu
na sehemu zilizotajwa hapo juu pamoja na kuimarisha usalama julisheni
kwa message kupitia namba hii
0783034224 na kwa simu ya
mdomo namba hii
0754034224 au
0787034224.
Namba hizi ni za mkuu wa Upelelezi
Kanda maalum.
Lengo la maelezo si vitisho kwenu bali ni tahadhari muhimu,
inayofaa kuzingatiwa,
S. H. Kova - SACP
KAMANDA WA KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
|